Monday, August 25, 2014

TAZAMA VIDEO KALI KUTOKA KWA SILVANUS ABEL MSUYA[ SILVABEL] MWIMBAJI WA NYIMBOZA INJILI ANAPASWA KUISHI MAISHA YANAYOENDANA UJUMBE ANAOHUBIRI KWENYE NYIMBO ZAKE KWA MAWASILIANO PIGA NO: +255717499962



NAMBA YA SILVANUS ABEL MSUYA 0717499962







Mwimbaji wa nyimboza injili anapaswa kuishi maisha yanayoendana ujumbe anaohubiri kwenye nyimbo zake
Silvanus Abel Msuya,mwimbaji,historia matukio

 
SILVANUS ABEL MSUYA


MUZIKI wa injili ni moja ya mziki ambao unapendwa kwa kiasi kibwa na watu wa rika zote  nchini Tanzania hasa kwa akinamama  na akinababa, kutokana na mziki huo kuimbwa katika mahadhi tofauti ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo mziki huo ulikosa watu wenye ubunifu hali ambayo ilipelekea kupigwa kanisani pekee.

Wapo wasinii wengi wakubwa ambao wamejikita  toka muda mrefu katika mziki wa injili {gosple},lakini ujio wa wasanii wengi chipukizi wenye vipaji na waliosomea mziki akiwemo Silvanus Abel Msuya imepelekea wasanii wengi kuwa wabunifu na  kutumia akali katika kutunga na kuimba nyimbo mbali mbali za injili hapa nchini.

Msuya ambaye ni mzaliwa wa kilimanjaro wilayani mwanga eneo la Ugeno{upare}  licha ya kuwa na kipaji cha kuimba, nyota yake ilianza kung'aa baada ya kuitimu mafunzo ya mziki katika chuo cha sanaa cha bagamoyo mwaka  2007,hali ambayo ilimshawishi baba yake mzee msuya kumpeleka nchini India kwenda kujiendeleza kimziki na kusomea mambo ya film and Television production katika chuo cha Asian Academy of Film and Television {AAFT} chini  ya Punjab Technical University  ambapo ilikuwa ni mwaka 2007 adi 2009,katika mzungumzo maalum  na championi Ijumaa anafafanua mengi kuhusu mziki wa injili hapa Tanzania ambapo yafuatayo ni maojiano maalum ambayo aliyafanya na mwandishi wa gazeti la championi pamoja Jelambaviwanjani.blogspot.com, hapa nchini Alex mapunda:-

Harakati zako za  kuimba zilianza lini,na wapi?

Mimi nilianza kuimba kabla ya kwenda kusomea mziki katika chuo cha sanaa bagamoyo 2007 lakini nilipokuwa india nilipata umaarufu mkubwa katika kumbi mbali mbali za mziki ambapo ilipelekea kujizolea mashabiki wengi sana na jina langu lilikuwa maarufu hasa chuoni kwetu,kwa kipindi hicho nilikuwa nikiimba mziki mchanganyiko.

Pia baada ya kurudi toka  India hapo ndipo nikatoa albamu yangu ya kwanza ambayo adi hivi sasa bado inafanya vizuri sokoni,licha ya kuachia albamu nyingine.

Albamu yako ya kwanza  ina nyimbo ngapi na akina nani umewashirikisha?.

Mimi ninakundi langu ambalo linafahamika kwa jina la Silvabel and the Melodians ambapo nipo mimi  mama yangu Haika Abeil Msuya,Mariam Damson Pamoja na Josephine Josephine,na albamu ambayo nilitoa mwaka 2009 ambayo inafanya vizuri adi hivi sasa inaitwa Yeova u Mwema na ina nyimbo 8.  




Nyimbo hizo ni yeova yu mwema,Si wa zamani {Rmx},Yesu akubari wakosaji pamoja na Inuka ushike kazi.

nyingine ni Tanzania nakupenda,nainua macho,Mungu Tusikie na wimbo wa mwisho unakwenda kwa jina la nakukaza Mrungu ambapo nyimbo zote zimefanyiwa video, Adox vidios 2010,pia nipo njiani kuachia albamu mbili moja wapo inaitwa Bwana ni mchungaji wangu ina  nyimbo 13 ambazo nimeziimba kwa umahili mkubwa sana,na nyigine yenye nyimbo sita ambazo nimeimba kwa lugha ya Kipare lugha ya kabira langu.

Ni vitu gani vimekuwa kikwanzo kwako toka ulipoanza Mziki adi hivi sasa?

Kwa kweli mziki wa Tanzania kwa sisi wasanii wachanga tunakubwa na matatizo mengi sana,mimi nafanya mziki wa injili ambao utoa ujumbe wa mungu ili watu wapate kuokoka lakini cha kushangaza unaweza ukazuiwa kwenda kufanya shoo kwenye mkutano wa dini kwa mapenzi binafsi ya baadhi ya watu,ifike wakati watu waeshimu mziki wa injili,pia kwa wasambazaji wanadharau sana nyimbo za wasanii chipukizi hata kama umeimba vizuri hali ambayo inakatisha tamaa kwa wasanii wadogo.


Kitu kingine ambapo kinanikwamisha ni majungu watanzania tulio wengi ni wanafiki sana na tunapenda kuzungumzia vitu bila kufanya utafiti,mara kadhaa baadhi ya watu wamewai kunishutumu kuwa ninamhusiano ya kimapenzi na wanakikundi wangu kwa kuwa saa nyingine shoo za mziki zinaisha usiku ili kunichafulia jina langu  kwa kweli niliumia sana lakini mungu akanipa ujasiri adi leo naendelea vizuri.



Mafanikio gani umepata Kupitia mziki wa injili?

Mafanikio makubwa ambayo nimeyapata katika mziki wa injili ni watu wengi wameokoka na wamepata uponyaji wa yesu kupitia nyimbo zangu ambapo, mara nyingi napigiwa simu toka maeneo tofauti  na watu mbali mbali ambapo wameupokea mziki ambao naimba kuna kipindi tulipata mwaliko wa kwenda zimbambwe watu walifurahi sana kutokana na haina ya mziki ambao naimba.

Zaidi ya hapo licha ya kupata fedha ambazo zinanisaidia kuendisha maisha yangu na kujilipia elimu ya masomo ya juu bado sijapata mafanikio  nawaomba watanzania wazidi kuniunga mkono.


kwa nini Gospel na  sio taarabu?

Kwanza mimi nimezaliwa katika familia ya kichungaji na nimelelewa kwa kufuata misingi ya yesu hivyo toka nilipokuwa mdogo nilikuwa na ndoto ya kuimba mziki wa injili,pia mimi spendi kuona kizazi chetu kinaangamizwa na shetani hivyo niliamua kwenda kosomea mziki ili niweze kuimba nyimbo bora zenye uponyaji wa bwana.

Nani alikushawishi kuingia kwenye tasnia ya mziki badala ya kilimo?.

Toka nilipokuwa mdogo nilikuwa nasikiliza sana nyimbo za bob maley,Jim Reeves pamoja na Jackon bandi,na nikanza kufuata nyayo zao hadi leo naimba,lakini kuhusu kilimo hilo bado nalifikiria kwa mapana lakini kipaji changu ni kuimba.

Kabla ya kuwa msanii maisha yako kabla yalikuwaje?

Kweli mungu ni mtu wa ajabu sana,mimi n nilikuwa mtukutu sana licha ya kuzaliwa katika familia ya kichungaji,nilikuwa mlevi,mwinzi na hata nilipokuwa India kunakipindi nilinusulia kwenda jela kwa matumizi ya bangi pamoja na kesi za wizi nashukuru mungu baadae nikaokoka na sasa mimi ni mtu mwema na namtumikia bwana.


Unaushauri gani kwa wasanii wote wa Tanzania?

Watu wanadhani mziki ni sawa na mchezo wa bao kila mtu anaweza akacheza,sio kweli mziki ni kazi na ili kufanya vinzuri watu wanatakiwa waendi darasani kusomea mziki huo,wapo wasanii wengi wazuri lakini hawana elimu unamkuta msanii hajui kupiga hata chombo kimoja cha mziki hii ni haibu kubwa.

Nje ya mziki kitu gani kingine unakifanya?

Mimi ni mwanachuo wa mwaka wa kwanza chuo kikuu cha iringa nasomea uandishi wa Habari,umri wangu ni miaka 30,nina mtoto Mmoja bado sijaoa,Anaitisha silvanus Msuya,ambapo kwa lolote la kuzungumza nae, namba yake ya simu ni0717499962,ili uweze kupata uponyaji kupitia nyimbo zake.

Mwisho.  

Sunday, August 24, 2014

MWIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI\ GOSPEL HAPA NCHINI ,WASILIANA NAE KWA SIMU NAMBA 0717499962.TANZAMA VIDEO ZAKE KALI.





NYIMBO AMBAZO ZIPO SOKONI KWA HIVI SASA.
1=VIDEO
2=AUDIO

NI PAMOJA NA................
  • MIMI NATANGAZA
  • BWANA U MWEMA
  • MUNGU YU MWEMA
  • INUKA USHIKE
  • TANZANIA NAKUPENDA
  • NAINUA MACHO JUU
  • MUNGU TWAOMBA
NAKUKAZA MRUNGU